DODOMA-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili jijini Dodoma kushiriki Vikao vya kikatiba vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya Taifa.
Katika uwanja wa ndege wa Dodoma amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Rosemary Senyamule na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama wa Mkoa huo.





