Jukwaa la kwanza wakuu wa taasisi za umma Zanzibar kuanza Mei 11

ZANZIBAR-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar imeandaa jukwaa la kwanza la wakuu wa taasisi za uwekezaji wa umma litakalofanyika kwa siku tatu kuanzia Mei 11 hadi 13, 2025 katika hoteli ya Golden Tulip Airport iliyopo visiwani humo.
Msajili wa Hazina Zanzibar, Bw. Waheed Mohammad Ibrahim Sanya amesema hayo leo Jumamosi Mei 3, 2025.

Amesema kuwa, lengo kuu la jukwaa hilo ni kuwaunganisha wakuu wa taasisi kutoka taasisi mbalimbali za umma ili kujadili changamoto za pamoja, kubadilishana uzoefu, na kuanzisha mikakati ya pamoja ya kuboresha utendaji wa taasisi zao.
“Kupitia jukwaa hili, wakuu wa taasisi za umma wataweza kuimarisha ushirikiano, kubadilishana maarifa, na kuchochea ubunifu,” alisema huku akitabanaisha kuwa mgeni rasmi atakuwa Mhe. Hemed Suleiman Abdullah, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Kaulimbiu ya Jukwa hilo ni “Uongozi Bunifu na Mashirikiano ni Muhimu ili kufikia Maendeleo Endelevu Zanzibar.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news