DAR-Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), imezitaka kampuni za Bima nchini kuwa waaaminifu kwa kufanya kazi kwa weledi na kulipa fidia kwa wateja wao, ili kujenga imani kwa maendeleo ya Taifa.
Naibu Kamishina wa Bima Tanzania, Khadija Said ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa Akiba Flex Plan ya Jubilee Life Insuarance na kuongezea kuwa wasikengeuke taratibu walizowekewa na mamlaka hiyo.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Insuarance, Helena Mzena amesema bima hiyo itamsaidia Mtanzania kumpa ulinzi, utu na amani hivyo kufanya bima ya maisha kuwa rahisi na kutoa mafao yake pale atakapoyahitaji.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























