Mtendaji Mkuu wa Mahakama awataka wahasibu kuandaa taarifa zenye viwango vya Kimataifa

NA MARY GWERA
Mahakama

MTENDAJI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel ametoa rai kwa Wahasibu wa Mahakama nchini kufanya kazi zao kwa weledi na kuandaa taarifa zenye viwango vya kimataifa ili kuusaidia Mhimili huo kutokuwa na hoja za kikaguzi.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua mafunzo ya Wahasibu wa Mahakama waliyotoka Kanda mbalimbali za Mahakama nchi nzima, mafunzo hayo yanafanyika katika jengo la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma leo tarehe 26 Mei, 2025.
Akifungua Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Wahasibu wa Mahakama ya Tanzania leo tarehe 26 Mei, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Prof. Ole Gabriel amesema kuwa, Mahakama imeaandaa mafunzo hayo kwa lengo la kuboresha uandaaji wa hesabu kwa viwango vya kimataifa (IPSAS) na kuwajengea uwezo Wahasibu katika eneo la uchambuzi wa taarifa za fedha.
Mhasibu Mkuu wa Mahakama ya Tanzania CPA Joseph Elikana akitoa neno fupi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wahasibu jijini Dodoma leo tarehe 26 Mei, 2025.

“Ndoto yetu kwakweli ndani ya Mahakama ya Tanzania ni ifike mahali tusiwe na changamoto yoyote ya masuala ya kikaguzi yaani tuwe ‘audit querry free’ na inawezekana, sasa rai yangu tu ni kwamba haya yanawezekana pale tu ambapo tunawekeza katika mafunzo na tunapodhani mafunzo ni ghali inatugharimu hasa katika uaandaji wa taarifa za kimataifa,” amesema Prof. Ole Gabriel.

Mtendaji Mkuu amesema kuwa, Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali chini ya uongozi wa Charles Kichere nayo inahitaji taarifa za kikaguzi za kihesabu zizoendana na viwango vya kimataifa na taarifa hizo zinahusisha pia taarifa za rasilimaliwatu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kadhalika,” amesema Prof. Ole Gabriel.

Ameongeza kuwa, ili kuendana na maendeleo ya teknolojia na ya kitaaluma, Mahakama imeona kuwa ni vema kuandaa mafunzo hayo kwa Wahasibu wa ngazi zote za Mahakama kuanzia Mahakama za Mwanzo hadi Rufani ili kuwawezesha kutanua wigo wa uelewa wa kutoa taarifa za kihasibu pamoja na kuendana viwango vinatakiwa na Serikali hususani Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo Bi. Patricia Ngungulu akitoa neno fupi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wahasibu jijini Dodoma leo tarehe 26 Mei, 2025.
Sehemu ya Wahasibu wakimsikiliza mwezeshaji kutoka water price coopers akitoa mada kwa wahasibu.
Sehemu ya Wahasibu wakimsikiliza mwezeshaji kutoka water price coopers akitoa mada kwa wahasibu.
Prof. Ole Gabriel ameeleza kuwa, Ripoti za ukaguzi za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinaonesha kuwa, kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita Mahakama imekuwa ikipata Hati ya kuridhisha katika matumizi ya miongozo ya ukaguzi kwa viwango vya kimataifa (Compliance with IPSAS).

“Hata hivyo, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali amekuwa akiainisha mapungufu kadhaa kwenye hesabu zetu ambayo ni pamoja na kutotumia ipasavyo moduli ya inventories ya ‘MUSE’ katika kusimamia mali za Mahakama, kutokuwa na nyaraka za kuthibitisha bakaa ya mali/bidhaa baada ya kuhesabu mali (stock taking) kwenye Mahakama za Mwanzo na Wilaya na nyingine kadhaa, kutowasilishwa hesabu kwa wakati kwa kuzingatia tarehe zilizowekwa” amesema Mtendaji Mkuu.

Amesema kuwa mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa washiriki 203 ambao ni Wahasibu na Viongozi katika ngazi za utawala. Washiriki hao wanatarajiwa kufundishwa jumla ya Moduli 12.

Prof. Ole Gabriel ameongeza kuwa, dhamira ya Mahakama ni kuhakikisha kwamba, watumishi wanawezeshwa vema na katika masuala mbalimbali ya kitaaluma yanayolenga kuwajengea uwezo ili watekeleze majukumu yao kwa weledi na ufanisi.

“Nitoe rai na kuwataka kuwa na utulivu na kushiriki mafunzo kikamilifu kwa kipindi chote mtakachokuwa hapa. Ni imani yangu kuwa baada ya mafunzo haya, ubora wa uandaaji wa ripoti za hesabu utaongezeka” amesisitiza.
Sehemu ya Wahasibu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akitoa mada kwa wahasibu.
Sehemu ya Wahasibu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akitoa mada kwa wahasibu.
Kadhalika, Mtendaji Mkuu huyo amewataka Wahasibu kujiendeleza kitaaluma hususani ya na kwamba ofisi yake iko tayari kushirikiana na wenye nia ya kuongeza maarifa ya taaluma hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Usimamizi wa Fedha, Bw. Joseph Elikana amesema kuwa, amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia vema maarifa ya watakayopata kuboresha utendaji kazi wao.

Kadhalika, Bw. Elikana amemshukuru Mtendaji Mkuu wa Mahakama kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ambayo yataboresha utendaji kazi za kihasibu.
Sehemu ya Wahasibu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akitoa mada kwa wahasibu.
Sehemu ya Wahasibu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akitoa mada kwa wahasibu.(Picha na INNOCENT KANSHA- Mahakama).

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu amesema kuwa, Nitoe taarifa kuwa, washiriki wa mafunzo hayo wamepangwa kuhudhuria katika makundi manne (4) ambapo mafunzo ya ‘Accounting Capacity Building’ watahudhuria kwa siku mbili kwa kila kundi la washiriki 49, kundi la pili 48, kundi la tatu 49 na kundi la nne la mafunzo ya ‘Data Analytics’ watahudhuria washiriki wote 57.

“Makundi matatu ya mwanzo yatafanya mafunzo kuanzia leo tarehe 26 Mei, 2025 hadi 31 Mei, 2025 na kundi la nne litahudhuria kwa siku moja ya tarehe 02 Juni, 2025,” amesema Bi. Patricia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news