DAR-Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Faustina Mfinanga (Nandy) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Label ya Muziki ya TheAfricanPrincess amethibitisha rasmi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa ameachana na Msanii wake Yammi aliyekuwa chini ya label hiyo, baada ya kumaliza mkataba wake kwa makubaliano ya pande mbili.
Nandy alimtambulisha Yammi kama msanii wake wa kwanza kwenye label hiyo Januari, 2023 hivyo kusimamia kazi zake za muziki na kuhudumu kwa kipindi cha miaka miwili.

