ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemkabidhi Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Zubeir Ali Maulid, Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/2024 ulioishia Juni 2024.

