KILIMANJARO-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki maziko ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Cleopa David Msuya yaliyofanyika nyumbani kwake Kijiji cha Chomvu, Usangi wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro leo Mei 13, 2025.



















