ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezitaka familia kuweka dhamira ya kusimamia malezi ya vijana na watoto ili kuwa na Taifa lenye heshima na maadili.

Dkt.Mwinyi amesema, mambo mengi yanayojiri sasa ndani ya jamii yakiwemo ya wizi na uharibifu wa miundonbinu ya Serikali yanafanywa na vijana waliokosa malezi bora na Maadili ya Dini.
Amesema kuwa,mustakabali wa nchi yoyote unahitaji malezi ya vijana na watoto waliolelewa kwa maadili ili kuwa watu wema na wazalendo wa nchi yao.
Ameeleza kuwa, ni lazima kila mmoja kuwa na dhamira ya kusimamia malezi ya vijana ndani ya familia ili kuwa na watu wema watakaokuwa viongozi wa baadae.
Rais Dkt.Mwinyi amewakumbusha waumini hao umuhimu wa kuendelea kuiombea nchi amani hasa wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba,mwaka huu.
Amesitiza kuwa,bado Serikali inakusudia kutekeleza mambo mengi zaidi ya maendeleo katika nyanja tofauti,hivyo suala la kuwepo kwa amani ndio kipaumbele muhimu zaidi .