ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo kama ifuatavyo;
Mosi, Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt. Mahmoud Dhamir Kombo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo.
Pili Dkt. Abdallah Ibrahim Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo (ZALIRI).
Tatu Dkt. Taliba Saleh Suleiman ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo (ZALIRI).
Pia,ndugu Shaaban Salum Jabir ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo (ZALIRI).Uteuzi huo unaanza leo Mei 2,2025.

