Rais Dkt.Mwinyi kumwakilisha Rais Dkt.Samia mkutano wa SADC nchini Zimbabwe

HARARE-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Zanzibar na kuwasili nchini Zimbabwe kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Rais Dkt. Mwinyi, akiambatana na Mkewe, Mhe. Mama Mariam Mwinyi, alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, jijini Harare, na Balozi wa Tanzania nchini humo, Balozi CP Suzan Kaganda.
Rais Dkt. Mwinyi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano huo ambao utajadili Mwongozo na Uhifadhi Endelevu wa Biashara ya Kaboni katika nchi wanachama wa SADC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news