Rais Dkt.Samia awaheshimisha wamachinga Dodoma, wasema asante

DODOMA-Umoja wa Wanawake Machinga Dodoma (UWAMADO) wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa soko la kisasa la Machinga Complex na miundombinu ya kisasa ya soko hilo ambalo ni la kipekee nchini.
Hayo yamesemwa jana wakati wa uzinduzi wa Chama cha UWAMADO uliofanyika kwenye eneo la Soko la Machinga Complex kwa kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule.
Akisoma risala katika hafla hiyo,Katibu wa UWAMADO, Bi. Mariam Kajembe amesema, umoja huo umelenga kuwaleta wanawake wamachinga pamoja ili kujijenga na kujiimarisha kiuchumi.

Pia UWAMADO umempongeza,Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa Soko la Machinga Complex ambalo limesaidia kuwaleta pamoja wafanyabiashara wengi wadogo pamoja ambao awali hawakuwa katika maeneo rasmi na hivyo kuwafanya kutokuwa rasmi.

Akitoa hotuba yake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule amewapongeza UWAMADO kwa kuamua kuanzisha umoja wao ambao utawasaidia kujiendeleza zaidi na kujiimarisha kiuchumi.
“Jambo hili la kuanzisha umoja ni jambo jema,hakikisheni umoja unafikia malengo mliyokusudia.

"Mheshimiwa Rais kawajengea soko kubwa na zuri,soko hili liwe kichocheo cha ukuaji wenu kimtaji na kibiashara.

"Niwatake uongozi wa Jiji la Dodoma kuendelea kubuni na kuanzisha maeneo mapya ya kuwapanga vizuri wafanyabiashara wadogo wa Dodoma,"alisema Senyamule.
Akitoa salamu zake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mheshimiwa Anthony Mavunde amewapongeza UWAMADO kwa kuona umuhimu wa kukaa pamoja kujiinua kiuchumi na kuwataka kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Jiji ambayo kiasi cha Shilingi Bilioni 7 kimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha wakina mama,vijana na watu wenye ulemavu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news