Shamira akabidhi samani za ofisi kwa UVCCM Manyara

MANYARA-Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Viti vitatu Bara, ndugu Shamira Mshangama akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa jumuiya hiyo na kuhamasisha ushiriki wa vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.
Shamira alitembelea ofisi ya UVCCM Mkoa wa Manyara kufanya kikao kifupi cha ndani, na kukabidhi samani za ofisi kwa UVCCM Mkoa wa Manyara iliyopokelewa na Katibu wa CCM Mkoa, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Comrade Enyasi Inyasi A. Amsi pamoja na wajumbe wengine wa kamati ya utekelezaji ngazi ya mkoa na wilaya.
Akiwa Manyara alipata nafasi ya kushiriki katika ziara ya Kamati ya Utekelezaji inayoongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Manyara,ndugu Inyasi S.Amsi, ziara iliyofanyika wilaya ya Kiteto na kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo:

Kufanya kikao cha ndani cha wajumbe wa baraza la UVCCM Wilaya ya Kiteto,kutembelea Shule ya Sekondari Engusero na kutoa zawadi ya Vifaa vya Michezo, kutembelea waasisi na mabalozi wa Chama, kushiriki mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Dosidosi.
Pia katika ziara hiyo Shamira pamoja na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa kutoka Mkoa wa Manyara Ndg. Christine Millya walichangia kiasi cha Shilingi 700,000 kwa ajili ya kuhamasisha na kuunga mkono shughuli za Vijana katika eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news