Steven Mukwala aiokoa Simba SC dhidi ya Singida Black Stars

DAR-Bao pekee lililofungwa na Steven Mukwala limetosha kuipa Simba SC alama tatu mbele ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Mtanange huo umepigwa Mei 28,2025 katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Awali, Simba SC walianza mchezo huo kwa kasi huku wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga, walikosa umakini wakuzitumia.

Mukwala aliwapatia bao hilo pekee dakika ya 42 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jean Charles Ahoua na kuwazidi ujanja walinzi wa Singida.

Dakika 15 za mwanzo za kipindi cha pili Singida walifika mara kadha langoni mwa Simba SC, lakini safu yao ya ulinzi ilikuwa imara kuondoa hatari zote.

Kwa ushindi huo Simba SC inafikisha alama 72 baada ya kucheza mechi 27 wakiendelea kusalia nafasi ya pili alama moja nyuma ya vinara Yanga SC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news