TAKUKURU yaokoa mapato ya mauzo ardhi ya kijiji

PWANI-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani katika kipindi cha Januari hadi Machi,2025 imefanikiwa kuokoa mapato ya asilimia 10 ya mauzo ya ardhi ya Halmashauri ya Kijiji cha Msufini Kidete wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti feki ya kijiji hicho iliyoghushiwa na mwanasheria wa kampuni iliyouziwa eneo la kijiji.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Domina Mukama ameyasema hayo Mei 29,2025 alipozungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano ulipofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisini kwake.

Kamanda ametaja jina la kampuni hiyo kuwa ni Brilliant Sanitary Ware Company Limited ambapo yalifanyika malipo ya shilingi milioni 385 wakiamini kuwa wanalipa ushuru wa Kijiji cha Msufini katika akaunti halali ya kijiji kumbe ilikuwa ni akaunti ya Mwanasheria

"Halmashauri ya Kijiji ilitakiwa kulipwa shilingi milioni 385 kama asilimia 10 ya mauzo ambapo fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti feki yenye jina kama la akaunti ya kijiji iliyowasilishwa na Mwanasheria wa kampuni hiyo,"amesema Kamanda Mukama.

Aidha,baada ya kufanyika malipo Mwanasheria huyo alizitoa fedha zote na kuzifanyia matumizi binafsi.

Kamanda huyo amesema,TAKUKURU imefanikiwa kurejesha fedha zote shilingi milioni 385 serikalini kupitia Halmashauri ya Kijiji cha Msufini, na tayari fedha hizo zimepangiwa matumizi ya kujenga jumla ya madarasa mawili ya Shule ya Sekondari Mbezi Gogoni na madarasa mawili katika Shule ya Msufini.

Pia, fedha hizo zimejenga nyumba mbili za walimu, wamechimba matundu 12 ya vyoo kisima kirefu cha maji na ukarabati wa Zahanati ya Kijiji cha Msufini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news