Tanzania mwenyeji wa eLearning Africa

NA GODFREY NNKO

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Kongamano la 18 la Kimataifa na Maonesho kuhusu Elimu ya Kidijitali, Mafunzo na Ukuzaji wa Ujuzi (eLearning Africa).
Kongamano hilo ambalo litafanyika Mei 7 hadi 9,2025 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es litakuwa la pili kufanyika hapa nchini tangu liasisiwe mwaka 2005.

Ethiopia ndiyo taifa la kwanza kuwa mwenyeji wa kongamano hilo kubwa zaidi barani Afrika ambapo lilifanyika mwaka 2006 jijini Addis Ababa.

Mwaka 2007, Kenya walikuwa wenyeji wa kongamano hilo ambalo lilifanyikia jijini Nairobi, mwaka 2008 lilifanyika jijini Accra nchini Ghana, mwaka 2009 jijini Dakar nchini Senegal.

Aidha, Lusaka nchini Zambia lilifanyika mwaka 2010, mwaka 2011 likafanyika hapa nchini jijini Dar es Salaam, jijini Cotonou nchini Benin mwaka 2012.

Windhoek nchini Namibia mwaka 2013 walikuwa wenyeji,Kampala nchini Uganda mwaka 2014, Addis Ababa walikuwa wenyeji tena mwaka 2015.

Kwa upande wa Cairo nchini Misri walikuwa wenyeji mwaka 2016, Port Louis nchini Mauritius mwaka 2017, Kigali nchini Rwanda mwaka 2018,Abidjan nchini Ivory Coast mwaka 2019, kwa mwaka 2020 na 2021 kongamano lilifanyika kwa njia ya mtandao kutokana na changamoto ya Uviko-19.

Kigali ilikuwa mwenyeji tena wa kongamano hilo mwaka 2022,Dakar mwaka 2023, Kigali ikawa mwenyeji tena mwaka 2024.

eLearning Africa ni kongamano na maonesho ya kila mwaka ambayo huwa yanawakutanisha maelfu ya wataalamu na wadau mbalimbali kubadilishana ujuzi na maarifa kuhusu elimu ya kidijitali barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news