Tanzania yatwaa tuzo nyingi kupitia Sekta ya Utalii

DODOMA-Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana amesema,Tanzania imeendelea kung’ara kwa kushinda Tuzo mbalimbali mbalimbali za utalii katika nyanja za Kimataifa.
Ameyasema hayo leo Mei 19,2025 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

"Hatua hiyo imedhihirishwa kwa mafanikio ya kishindo kwa kupata Tuzo maarufu Duniani za World Travel Awards (WTA) zinazotolewa na Taasisi ya World Luxury Media Group Limited ya nchini Uingereza katika msingi wa kutambua na kutangaza ubora wa vivutio na huduma za utalii, ambapo Tanzania imeshinda Tuzo saba za Kimataifa.

"Tuzo hizi zimeendelea kuwa chachu ya kujitangaza na kutambulika katika majukwaa ya kimataifa na kuchagiza ongezeko la idadi ya watalii wanaotembelea nchini."

Kwa upande mwingine, Waziri Chana amesema,Tanzania imepewa hadhi ya kuwa mwenyeji wa Tuzo za World Travel Awards kwa Kanda ya Afrika zitakazotolewa mwezi Juni, 2025.

Vilevile, amesema katika kutambua na kuhamasisha wadau kuendeleza uhifadhi na utalii,wizara imezindua tuzo maalum zilizojulikana kama The Serengeti Awards zenye lengo la kutambua mchango wa wadau katika kuendeleza uhifadhi na kutangaza utalii.

"Uzinduzi wa tuzo hii ulifanyika Disemba, 2024 jijini Arusha na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 500 ambapo miongoni mwa watu mashuhuri waliopata Tuzo ni Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan (Tuzo ya Kiongozi Mwenye Maono yaani Visionary Leadership Award).

"Mhe. Zakia Hamdani Meghji,Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na familia ya mgunduzi
mashuhuri duniani wa zamadamu Louis na Mary Leakey."

Amesema,tuzo hizo zitaendelea kuimarishwa na kutolewa kila mwaka ili kuendelea kuhamasisha na kutambua michango mbalimbali ya wadau wa Sekta ya Maliasili na Utalii."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news