TMA yaendelea kuzipiga msasa taasisi za hali ya hewa Afrika,sasa ni zamu ya Zimbabwe

DAR-Leo Mei 20,2025 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepata ugeni kutoka Idara ya Huduma za Hali ya Hewa (MSD) ya Zimbabwe ambao umekuja kuwatembelea na kujifunza masuala mbalimbali ya huduma za hali ya hewa Tanzania. 
Ugeni huo umeichagua TMA kwa ajili ya kuja kujifunza na kutambua maendeleo na mchango mkubwa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika kuimarisha huduma za hali ya hewa barani Afrika.

Kuhusu TMA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilianzishwa kwa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Na.2 ya mwaka 2019 kupitia Tangazo la Serikali GN 459 la Tarehe 14 Juni 2019. Ikiwa na jukumu la kuratibu, kudhibiti na kutoa huduma za hali ya hewa patika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mamlaka hii inatokana na ulokuwa wakala wa hali ya hewa Tanzania ulionzishwa kwa sheria ya wakala (Executive Agency Act) sura Na. 245 marejeo ya Mwakatuma 2022. 

Kabla ya wakala wa hali ya hewa huduma za hali ya hewa nchini zilikuwa zinatolewa na iliyokuwa idara ya Hali ya Hewa nchini (Directorate of Meteorology) ambayo ilianzishwa mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikiwa na jukumu la kufanya uangazi na kutoa taarifa za hali ya hewa nchini.

Kabla ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huduma za hali ya hewa nchini zilitolewa chini ya Taasisi ya hali ya hewa iliyokuwa chini ya wakoloni.

Aidha,mamlaka ambayo ipo chini ya Wizara ya Uchukuzi Tanzania inamiliki Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kilichopo Kigoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news