Tuendelee kudumisha amani kwa umoja na mshikamano nchini-Rais Dkt.Mwinyi

DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewasihi wananchi wa Tanzania kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na amani kwa mustakabali mwema wa Taifa kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo na kujiepusha na matendo yanayoweza kuleta mgawanyiko.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipofungua Dua Maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Mamufti, Masheikh, na Waislamu waliotangulia mbele ya haki iliofanyika katika Msikiti wa Mohamed VI-Bakwata Makao Makuu, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Mei 8,2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza Uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kuendeleza utaratibu wa dua ya kila mwaka na kuiombea nchi amani.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, amani ina umuhimu mkubwa katika Uchaguzi Mkuu Mwaka huu kabla, wakati na baada ya uchaguzi huo.

Rais Dkt.Mwinyi amesema, jukumu la kuwaombea Dua Masheikh, Walimu, na Waislamu waliohai na waliotangulia mbele ya haki na kuiombea amani nchi ni miongoni mwa dalili za imani ya kweli kwa waumini wa Dini ya Kiislamu kwa mikusanyiko yenye heri kwa mustakabali wa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news