Tume yatangaza majimbo mapya ya uchaguzi 2025

DODOMA-Kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa kwa pamoja na kifungu cha 10(1)(d) cha Sheria,ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na.2 ya Mwaka 2024,Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka na jukumu la kuchunguza, kupitia mipaka na kugawamajimbo ya uchaguzi katika Jamhuri ya Muungano.

Aidha, kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 18(1) ya Kanuni za Tume Huru yaTaifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, kupitia vyombo vya habari, Tume ilitoa tangazo kuutaarifu umma kuhusu kuanza kwa mchakato wa kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi kuanzia tarehe 27 Februari hadi 26 Machi, 2025.

Tangazo hilo liliweka utaratibu na vigezo vitakavyozingatiwa na Tume wakati wa kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi. Kufuatia tangazo hilo Tume ilipokea jumla ya maombi thelathini na nne (34) ya kugawa majimbo ya uchaguzi na maombi kumi (10) ya kubadili majina ya majimbo.

Baada ya kupokea maombi na kwa kuzingatia kanuni ya 18 (5) ya Kanuni za TumeHuru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, Tume ilitembelea na kufanya vikao na wadau katika baadhi ya majimbo yaliyoomba kugawanywa pamoja na majimbo yote;



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news