VIDEO:Fireman aibua hoja nzito Pwani, amuomba Spika kuingilia kati

PWANI-Mei 5,2025 Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba (Fireman) baada ya Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega kusoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Fireman ameibuka na hoja kadhaa huku pia akionesha kuuzunishwa na jengo la TRA analodai limetelekezwa.
Ni eneo la ofisi za TRA Vigwaza Kambini ambapo amesema, kwa miaka miwili ofisi hizo zimeshindikana kufunguliwa na kuishia kugeuka pagale.

Vilevile, amemuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson kuangalia namna ambavyo Bunge litaijadili barabara ya Morogoro kwa dharura kwani imekuwa changamoto kwa wananchi.

Amesema, licha ya Wizara ya Ujenzi kufanya vizuri katika miradi mbalimbali nchini, bado kuna miradi ambayo inahitaji kipaumbele ili kuokoa maisha ya Watanzania wengi nchini.

"Kwa sasa kuna viashiria vya wazi kuwa, watu wengi wapo hatarini kupata vilema na vifo katika babaraba ya Morogoro hususani kuanzia Kibaha, Mlandizi, Chalinze na Morogoro."

Amesema,ni miaka sasa imepita wadau na Serikali imekuwa ikizungumzia kuhusu juhudi za kuanzisha barabara ya ubia kati ya sekta binafsi na Serikali kuanzia Tamco, Maili Moja, Chalinze mpaka Morogoro.

Fireman amesema, awamu ya kwanza ya ujenzi huo ilitarajiwa kuishia Chalinze na awamu ya pili kuanzia Chalinze hadi Morogoro ambapo ilitarajiwa kutumia zaidi ya shilingi trilioni mbili.Tazama video chini》
Tazama video ya eneo la TRA chini》

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news