DAR-Katika kuendeleza ushirikiano wa kiutendaji kati ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) na Bodi ya Filamu Tanzania leo Ijumaa Mei 30,2025, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dkt. Gervas Kasiga wametembelea Kikundi cha Jambo na Vijambo ambacho kinajihusisha na utoaji wa elimu ya kijamii kwa vijana hususani kuhusu madhara ya dawa za kulevya.
Katika tukio hilo, Kamishna Jenerali Lyimo alieleza kufurahishwa kwake na kazi nzuri inayofanywa na Jambo na Vijambo katika kuelimisha jamii juu ya hatari za matumizi ya dawa za kulevya, huku akisisitiza kuwa juhudi kama hizo zina mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya tatizo hilo sugu.
Katika tukio hilo, Kamishna Jenerali Lyimo alieleza kufurahishwa kwake na kazi nzuri inayofanywa na Jambo na Vijambo katika kuelimisha jamii juu ya hatari za matumizi ya dawa za kulevya, huku akisisitiza kuwa juhudi kama hizo zina mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya tatizo hilo sugu.Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga, amemshukuru Kamishna Jenerali Lyimo kwa ushirikiano mkubwa anaoendelea kuutoa kwa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza katika juhudi za kupambana na dawa za kulevya.
Alibainisha kuwa ushirikiano kati ya DCEA na Bodi ya Filamu tayari umeanza kuzaa matunda, na kwamba wako tayari kuuimarisha zaidi ili kufanikisha mapambano haya kwa njia ya uelimishaji kupitia kazi za sanaa.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)









