Waziri Dkt.Nchemba aishukuru AfDB kwa kushiriki ujenzi Reli ya Kisasa (SGR)

ABIDJAN-Waziri wa Fedha, Mhe.Dkt.Mwigulu Nchemba (Mb), ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini ( Development Bank of Southern Africa), kwa kushiriki katika ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), mradi ambao ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania na nchi jirani zitakazonufaika na mnyororo wa thamani wa mradi huo wa kikanda.
Mhe. Dkt. Nchemba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bi. Buitumelo Mosako, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) iliyofanyika, Abidjan nchini Ivory Coast.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini (DBSA) kwa mchango wenu muhimu katika kufadhili ujenzi wa SGR kipande cha 3 na 4 (Makutupora hadi Isaka) kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 100. Zaidi ya hapo, tunatambua na kuthamini msaada wa kifedha wa kiasi cha dola milioni 100 uliotolewa awali kwa ajili ya kujenga kipande cha 2, ambao uliweka msingi imara kwa mradi mzima wa SGR” alisema Dkt. Nchemba.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DBSA, Bi. Buitumelo Mosako, alisema kuwa milango ya ushirikiano na Tanzania iko wazi na kwamba Benki yake ina subiri kukamilika kwa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ili waweze kuangalia maeneo ya kushirikiana.

Alisisitiza kuwa Benki yake iko tayari kuwekeza zaidi Tanzania katika kusaidia miradi ya kimkakati na kijamii katika sekta za m aji, afya, nishati, uchumi wa kidigitali, ujenzi wa makazi ya gharama nafuu na ujenzi wamiundombinu mbalimbali.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Msaidizi wa Baraza la Mawaziri, Bw. Fidelis Mkatte, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, pamoja na maafisa wengine waandamizi kutoka Serikali ya Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news