Wananchi wajifunza mengi kuhusu majukumu ya BoT maonesho ya Mbeya City Expo 2025

MBEYA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inashiriki Maonesho ya Mbeya City Expo 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Soko la Uhindini, kuanzia tarehe 23 hadi 31 Mei 2025.
Ushiriki wa BoT katika maonesho haya una lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yake mbalimbali katika kusimamia uchumi wa nchi.

Katika kipindi chote cha maonesho, wananchi wa Mkoa wa Mbeya na maeneo ya jirani wamekuwa wakipata elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayosimamiwa na Benki Kuu, yakiwemo usimamizi wa sera ya fedha, udhibiti wa mfumuko wa bei, usimamizi wa mabenki na taasisi za fedha, pamoja na elimu ya utambuzi wa alama za usalama katika noti na njia bora za utunzaji wa noti zetu.
Banda la BoT limevutia wageni mbalimbali, wakiwemo viongozi wa kitaifa na kimataifa. Miongoni mwa waliotembelea banda hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Juma Homera pamoja na Mabalozi wa Tanzania waliopo katika nchi jirani za Afrika, akiwemo Mhe. Agnes Kayola, Balozi wa Tanzania nchini Malawi; Mhe. Said Mshana, Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo; na Mhe. Lt. Gen. Mathew Mkingule, Balozi wa Tanzania nchini Zambia.
Benki Kuu hushiriki katika maonesho mbalimbali nchini kama sehemu ya juhudi za kuwafikia wananchi na kuwapa elimu, kwa lengo la kuongeza uelewa wao kuhusu majukumu yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news