NAIROBI-Hakika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajivunia kuwa na Kiongozi mwenye msimamo, mwenye hekima na anayejua kulinda maslahi ya taifa, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika mahojiano na Citizen TV ya Kenya, Waziri Kiongozi wa Kenya, Musalia Mudavadi, ameunga mkono msimamo wa Rais Samia dhidi ya wanaharakati kutoka nje wanaoingilia mambo ya ndani ya Tanzania.
“Sitaipinga kauli ya Rais Samia kwa sababu kuna ukweli ndani yake.Huku kwetu Kenya uhuru wa maoni umevuka mipaka,hakuna heshima tena,” alisema Mudavadi kwa uwazi mkubwa.
Awali,Rais Samia alieleza wazi kwamba baadhi ya wanaharakati wa kigeni wameanza kutumia migogoro ya kisiasa kama njia ya kuvuruga amani ya Tanzania, huku wengine wakitoka Kenya kufuatilia kesi ya Tundu Lissu kwa mtazamo wa kichokozi.
“Walishavuruga kwao, tusikubali waje kutuharibia huku. Nchi iliyobaki salama na yenye utulivu ni Tanzania,” alisisitiza Rais Samia.
🇹🇿 Tanzania si uwanja wa majaribio ya fujo na siasa za matusi.
🇹🇿 Serikali iko imara kulinda amani, utu, na hadhi ya nchi yetu.
🇹🇿 Wanaojifanya wanaharakati lakini lengo lao ni kuchochea vurugu hawana nafasi katika ardhi yetu.
■Tunasimama na Rais Samia.
■Tunasimama na amani ya Tanzania.
Tags
Habari
