Akiba Commercial Bank Plc yashirikiana na Chuo cha TIA kupanda miti 1,500

DAR-Benki ya Akiba Commercial Plc (ACB) kwa kushirikiana na Chuo cha Uhasibu (TIA), imepanda miti 1,500 katika kampasi ya TIA ya Kurasini ikiwa ni sehemu ya juhudi endelevu za kulinda mazingira chini ya mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Zoezi hilo limeongozwa na Afisa Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Bi.Wezi Mwazani ambapo amesema, hiyo ni dhamira thabiti kwa vitendo kuhusu imani ya benki katika suala la kulinda mazingira kwani ni jukumu la pamoja kati ya taasisi na wananchi.

"Tuko tayari kuendeleza mpango huu katika kampasi nyingine za TIA tutakapohitajika,”aliongeza, akisisitiza utayari wa ACB kuendelea kushiriki katika juhudi za kimazingira kote nchini.
Meneja Mwandamizi wa Huduma za Wateja Binafsi ACB, Bw.Emmanuel Mseti alitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa chuo hicho,wafanyakazi na wanafunzi wa TIA kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha kuwezesha kufanikisha tukio hilo.

“Zoezi hili si la ishara tu bali ni hatua ya vitendo inayoonesha dhamira yetu ya kulinda mazingira,ACB tunaamini katika kuchukua hatua halisi kupanda miti hadi kutoa huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali na mazingira ni kipaumbele chetu,” amesema Bw. Mseti.

Hata hivyo alieleza kuwa huduma za kidigitali za benki hiyo ACB Mobile, Internet Banking na Akiba Wakala zinaongeza upatikanaji wa huduma kwa ufanisi huku zikisaidia kupunguza matumizi ya karatasi, kuunga mkono mfumo wa kibenki unaolinda mazingira.
Bw. Mseti pia alitaja ushiriki mpana wa benki hiyo katika kulinda mazingira, ukiwemo mradi wa kuendeleza na kupendezesha uliofanyika Bustani ya Mnara wa Uhuru jijini Dodoma, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji ikiwa ni mfano wa mshikamano wa kweli na jamii.

"Kwa Benki ya Akiba Commercial, kujitoa kwa jamii si hiari bali ni wajibu. Kuanzia elimu, afya, ushirikishwaji wa kifedha hadi utunzaji wa mazingirabenki inaendelea kujenga mustakabali jumuishi na endelevu kwa Watanzania wote."

Aidha,aliwasisitiza na kuwatia moyo wanafunzi wa TIA kuenzi miti hiyo kwa kuitunza ili iwe urithi wa kizazi sasa na kijacho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news