DAR-Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Penuel Fm Radio,Alphonce Temba amechukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea Ubunge Jimbo la Kibamba mkoani Dar es Salaam.
Temba ambaye pia ni Mwinjilisti na Muhubiri wa Kimataifa amechukua fomu Juni 28,2025 na kukabidhiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo, Masunga Mwenge.


