DAR-Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Steven Mnguto amewasilisha barua ya kujiuzulu wadhifa huo.
Katika hatua nyingine taarifa ya Juni 13, iliyotolewa na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao imeeleza kuwa Rais wa TFF, Wallace Karia amemsimamisha kazi Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo.