Waziri Mkuu apeleka tabasamu kwa watoto Kituo cha Sanganiwa mkoani Kigoma

KIGOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tarehe 13 Juni, 2025 ametembelea kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Sanganigwa kilichopo mjini Kigoma, kinachosimamiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma.
Akizungumza na watoto na walezi wa kituo hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa, Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa madhehebu ya dini katika kuwalea kimwili na kiroho watoto wenye mahitaji maalum nchini.
“Kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ninalishukuru Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma, mtu mmoja mmoja na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa Serikali katika kuwalea watoto wetu, hakika mnafanya jambo kubwa na la kumpenda Mungu na wanadamu.”
Akisoma taarifa ya kituo hicho kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Kituo hicho Keneth Hageze amesema kuwa kilianzishwa mwaka 1995 na mpaka sasa kimehudumia watoto 1309.

Mheshimiwa Majaliwa alitoa Mchele, Maharage, Mafuta, Sukari pamoja na Taulo za kike.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news