CP Wakulyamba awapa somo maofisa na askari wanafunzi TANAPA

NA SIXMUND BAGASHE

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia masuala ya Uhifadhi, Kamishna wa Polisi,CP Benedict Wakulyamba ametoa semina elekezi kwa Maofisa na Askari Wanafunzi wa Kozi ya 11 ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Mlele mkoani Katavi.
Katika semina hiyo, CP Wakulyamba amesisitiza masuala muhimu yanayohusu utendaji kazi wenye weledi, mahusiano bora kazini, madhara ya utendaji mbovu, pamoja na kazi za msingi za uhifadhi wa maliasili.
Aidha, amewahimiza Maofisa na Askari hao kujiepusha na vitendo vya rushwa na maadili mabovu kazini, huku akiwataka wajikite kujifunza na kuelewa vyema sheria husika, hasa zile zinazohusu uhifadhi wa maliasili.

“Ni lazima mjiepushe na utendaji mbovu. jiepusheni na rushwa, mjenge mahusiano mema na wananchi. Mkitaka kufanikisha majukumu yenu, mshirikiane kwa karibu na wananchi hao,” amesisitiza CP Wakulyamba.
Semina hiyo ni sehemu ya maandalizi kuelekea kufungwa kwa mafunzo rasmi ya Maofisa na Askari 229 wa Jeshi la Uhifadhi kutoka TANAPA kesho Juni 10, 2025 katika kituo hicho cha Mlele.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news