MTWARA-Afisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Pwani, Bi. Salome Mbonile ametoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya kwa vijana wa Kampuni ya Ulinzi ya Assguard waliokuwa kwenye mafunzo ya kijeshi mkoani Mtwara.
Takribani washiriki 400 walifikiwa na kuelimishwa kuhusu athari za matumizi ya dawa za kulevya na umuhimu wa kutumia stadi za maisha waliyojifunza kwa njia chanya.
Aidha, walielezwa kuwa, matumizi ya dawa za kulevya yamezima ndoto za watu wengi, hivyo wana wajibu wa kushirikiana na jamii ikiwemo Serikali kupitia mamlaka katika kusaidia mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
"Lakini yule mraibu anapokosa dawa za kulevya anapata arosto,akipata arosto anataka apate dawa za kulevya.
"Kwa hiyo, mraibu ni mtu ambaye hawezi kuishi bila kutumia dawa za kulevya, kwa hiyo ndugu yako akipata tatizo kama hili inaumiza sana,fikiria amefariki kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya."
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)

