Dkt.Adesina awasili Tanzania kwa mazungumzo na Rais Dkt.Samia,uzinduzi wa miradi ya miundombinu

DAR-Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Akinwumi Adesina amewasili jijini Dar Es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku nne kuanzia tarehe 12 hadi 15 Juni 2025.
Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alipokewa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Mhe. Denis Londo.

Wakati wa ziara hiyo, Dkt. Adesina anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Dkt. Adesina na Rais Samia watashiriki hafla ya ufunguzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na barabara ya mzunguko ya Dodoma jijini Dodoma tarehe 14 Juni 2025.

Katika ziara hii, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kitamtunukia Shahada ya Heshima ya Falsafa Dkt. Adesina tarehe 13 Juni 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news