Zanzibar kuwa kituo bora cha utoaji huduma za usafiri wa anga-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema,Zanzibar inajipanga kuendelea kujenga miundombinu ya viwanja vya ndege ili kuiwezesha kuwa kituo bora cha utoaji wa huduma za usafiri wa anga.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua rasmi Mkutano wa Huduma za Usafiri wa Anga pamoja na Utalii Afrika, uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, iliyopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo tarehe 12 Juni 2025.
Ameeleza kuwa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na ujenzi wa Uwanja wa Ndege mpya wa Pemba ni miongoni mwa juhudi zinazochukuliwa na Serikali za kuimarisha huduma za usafiri wa anga nchini.

Rais Dkt. Mwinyi amefafanua kuwa hatua hiyo itaifungua Zanzibar kikanda na kimataifa kwa mashirika zaidi ya ndege kuja nchini, na hivyo kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea pamoja na kutangaza utalii wa Zanzibar.
Aidha, amesema huduma za usafiri wa anga ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa sekta ya utalii inayochangia asilimia 30 ya pato la taifa na kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa Zanzibar.

Aidha, Serikali inaendelea kushirikiana na sekta binafsi na mashirika ya ndege ya kikanda na kimataifa ili kuongeza ufanisi na usalama katika viwanja vya ndege.
Vile vile ameongeza kusema kuwa katika miaka ya karibuni kumeshuhudiwa ukuaji mkubwa wa sekta ya utalii, uliotokana na juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya Royal Tour iliyoitangaza Tanzania, ikiwemo Zanzibar, na kutambulika kwa vivutio vya utalii, utamaduni na urithi wa kihistoria.
Pia, amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha huduma katika viwanja vya ndege, ikiwemo kushirikiana na sekta binafsi kupitia sera ya PPP, mashirika ya ndege ya kikanda na kimataifa, pamoja na kusimamia ipasavyo kanuni na miongozo ya huduma za usafiri wa anga na hali ya usalama wa nchi hatua inayochangia kuongezeka kwa mashirika ya ndege yanayotoa huduma nchini.
Mkutano huo wa Kimataifa wa Masuala ya Anga na Utalii, maarufu kama AviaDev Africa 2025, umeanza ta

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news