Dkt.Biteko awasili Rwanda kushiriki Mkutano wa Nyuklia barani Afrika

KIGALI-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Doto Biteko Juni 29, 2025 amewasili Kigali nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano unaohusu masuala ya nyuklia Afrika.
Katika Mkutano huo unaotarajiwa kuanza Juni 30 hadi Julai 1, 2025 nchini humo unajumuisha wadau wa nishati kutoka ndani na nje ya Afrika wenye lengo la kuharakisha matumizi ya nyuklia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuleta mabadiliko ya nishati Afrika.
Pamoja na ushiriki wake katika Mkutano huo Dkt. Biteko anatarajiwa kufungua mjadala wenye mada kuhusu nishati Afrika na utashi wa kisiasa.

Aidha, katika Mkutano huo Dkt. Biteko ameambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkurugenzi wa Tume ya Mionzi ya Atomiki, Prof. Najat Mohamed.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news