MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango tarehe 07 Juni 2025 ameondoka nchini kuelekea Ufaransa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3), utakaofanyika jijini Nice, kuanzia tarehe 09 hadi 13 Juni, 2025.

Mkutano huo unawakutanisha Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Kimataifa, Asasi za Kiraia pamoja na Sekta binafsi.
Aidha, Makamu wa Rais anatarajiwa kushiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania, Mashirika na Mataifa yanayoshiriki Mkutano huo.