Fundi Makenika,Mhasibu wa Hospitali ya KKKT Orkosumet mahakamani kwa uhujumu uchumi na jinai

MANYARA-Juni 18,2025 Katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro imefunguliwa Kesi ya Uhujumu Uchumi Na 7343/2025 mbele ya Mhe. Onesmo Nicodemo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Wilaya ya Simanjiro dhidi ya Bw. Dominick Huphrey Mariki aliyekuwa fundi makenika wa Gereji ya Ushirikiano.
Mshtakiwa mwingine ni Bw. Charles Miseyeki Mhasibu wa Hospitali ya KKKT Orkosumet.

Washtakiwa wanashtakiwa kwa makosa ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Cap 329 R:E 2022.

Sambamba na kosa la Kughushi kinyume na kifungu cha 333, 335(a) na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Cap 16 R:E 2022.

Akisoma hati ya mashtaka Mwendesha mashtaka wa TAKUKURU,Bw.Faustin Mushi amesema,washtakiwa walitumia nyaraka za hati ya malipo kuonesha kuwa gari la Hospitali ya KKKT iliyopo Orkesumet limepelekwa gereji na kufanyiwa matengenezo ya shilingi milioni 6,163,000 huku wakijua kuwa gari hiyo haijafanyiwa matengenezo.

Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa namba mbili ambaye ni Bw.Dominick Humphrey Mariki kwa kufanya makubaliano (plea bargaining) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Ambapo mtuhumiwa huyo ametakiwa kulipa fidia ya shilingi milioni 3,081,503 na kutumikia kifungo cha nje cha miezi sita amabapo hadi sasa mshtakiwa ameshalipa fidia ya sh. 2,000,000 kwenye akaunti ya BoT ya DPP na kiasi cha sh.1,081,503 atatakiwa kulipa kabla ya Septemba 2,2025.

Shauri limepangwa kusikilizwa Julai 2,2025 ili kusikilizwa hoja ya Awali (PH) kwa ajili ya mshatikwa namba moja Bw.Charles Miseyeki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news