Tanzania yajitosa nafasi ya Ujumbe wa UNESCO

PARIS-Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimejitosa katika kuwania nafasi ya wajumbe wa kuunda kamati Jumuishi ya kiserikali ya kusimamia Utekelezaji wa mkataba wa UNESCO wa mwaka 2005 ambao unalenga kulinda na kuendeleza uanuai wa kijieleza kiutamaduni.
Dkt. Kedmon Mapana ambaye ni Mtendaji Mkuu wa BASATA ndiye mgombea kutoka Tanzania katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 20 Juni, 2025 ambapo yeye na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya sanaa Dkt. Emanuel Ishengoma wameshiriki katika Mkutano wa 10 wa Nchi wanachama wa UNESCO unaofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Paris, Ufaransa.

Aidha, kutakuwa na Faida Lukuki endapo Tanzania itashinda katika nafasi hiyo ya Ujumbe, ikiwa ni pamoja na kuwa na nafasi kubwa ya Kushiriki katika Majadiliano na maamuzi ya Kidunia yanayohusu Uanuai wa Utamaduni na pia kunufaika na miradi mbalimbali ya UNESCO.

Pia faida nyingine ni kusaidia kuhakikisha kila nchi inakuza na kulinda uanuai wa kitamaduni kwa kiwango cha kimataifa na kusaidia katika ufuatiliaji wa karibu wa kuhakikisha kila nchi mwanachama inaweka mazingira mazuri ya ulinzi wa uanuwai wa kitamaduni katika mila, desturi na Sanaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news