Msemaji Mkuu wa Serikali atoa pole ajali ya Same

DAR-Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki kufuatia ajali mbaya ya kugongana kwa mabasi mawili na kuunga moto iliyotokea katika eneo la Sabasaba Kata ya Same Mjini, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Juni 28, 2025 na kusababisha vifo vya watu 38.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa tarehe 29 Juni, 2025 ametoa taarifa ya Serikali kupitia mkutano na Waandishi wa Habari katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara; Sabasaba, Dar es Salaam ambapo amezungumzia masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali katika kuwaletea Watanzania maendeleo.

Msigwa ametoa salamu hizo za pole Juni 29, 2025 jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza familia zao na anaungana na familia zote katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

“Kwa masikitiko makubwa, katika ajali hii tumepoteza Watanzania wenzetu 38 na Wenzetu 28 wameumia. Moja ya mabasi haya aina ya Coaster lilibeba ndugu wa familia moja ambao walikuwa wanakwenda Moshi kwa shughuli ya kifamilia,”amesema Msigwa.

Ameongeza kuwa katika ajali hiyo wengi wa waliopteza maisha ni wale waliokuwa wanakwenda kwenye harusi mkoani Moshi ambapo pia madereva wote wawili wa mabasi hayo wamepoteza maisha.

"Nawaomba watumiaji wa barabara zetu hususani madereva wa magari na madereva wa bodaboda na watumiaji wote wa babarabara mzingatie na kuheshimu taratibu za usalama barabarani ili kuepusha ajali kama ambavyo pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyowasisitiza madereva kuendelea kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani akiliagiza Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia kikamilifu sheria hizo alipokuwa akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Juni 27, 2025 jijini Dodoma."

Katika hatua nyingine, Msigwa ameeleza kuwa, katika majeruhi 28, majeruhi 22 wametibiwa na kuruhusiwa na majeruhi sita wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya KCMC, Mawenzi na Same mkoani Kilimanjaro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news