SHUKRANI
Shalom shalom.Mimi nabii James Nyakia, Niko salama kabisa!Naendelea na majukum yangu ya kawaida maana Mungu yuko Rohoni mwangu!.
Asante sana Master King kwa upendo wako usiokuwa na kifani!.Jana ni wewe peke yako uliamua kuacha vyote ukaja kuungana na Mimi!
Hukuogopa kukamatwa, kudhalilika wala kufedheheshwa au kufedheheka! Ulichokiona ni upendo tu! Asante sana Master King! Nimejifunza kitu kwako!.
Asanteni sana wote mlioniombea na naamini hili litakwisha salama kwa mafunzo kwangu na nitakuwa na ustawi mkubwa sana sana baada ya hapa!.
Serikali yetu ipo kuturekebisha, sio kutuadhibu tu! Kuna wakati wao ni walimu na yatupsa kusikiliza na kutekeleza! Hata hili la kwangu litakwisha na nitakuwa bora zaidi!.
Wito wangu kwenu! Msitukebehi na kutucheka watumishi wenzenu tunaopitia katika changamoto ya aina Kama hii ya kwangu! Kikubwa ni kuombeana na Kama unafaham zaidi madhaifu yangu, Tuombeane!.
Asante sana kwa kipekee kwa Baba Mchungaji Anthony Lusekelo! Huyu ni baba! Kanijulia Hali kila wakati na kila siku tokea hili jambo limetokea! Asante sana na Mungu azidi kumpa afya njema!.
Asante wote mliopiga Magoti kuniombea, mimi nilie mkosaji kwa sasa ili Mungu anipe Rehema na Neema zake!.
Naamini, Serikali inakusudia kunisaidia nifanye vizuri zaidi kwa ubora na kwa ustawi zaidi na zaidi na nitafanya vizuri zaidi ya sasa kwa jina la Yesu!.
Wale mliofurahia pia, Nawaombea mema mazuri mazuri yazidi kuja kwenu kwa jina la Yesu!.
Mimi ni mnyenyekevu wakati wote na ni mtu wa kushuka mpaka majivuni na hata kwa kulala matopeni! Naamini, Serikali ya Tanzania inanipenda na inaniongoza vizuri na kwa miongozo yao mizuri nitafika mbali sana na dunia inanisubiri kwa jina la Yesu!.
Serikali haijawahi kumwacha mtu mnyenyekevu na msikivu, mimi ni msikivu na mnyenyekevu, itanisikiliza! Itaniongoza vema na itanisaidia kufika mbali zaidi katika utumishi wangu!.
Ninachoamini, Serikali yangu inataka nifanye vizuri zaidi ya hapa na inataka nifike mbali zaidi ya hapa nilipo! Niko tayari kuisikiliza na kutii na kutekeleza na kufanyia kazi kila maelekezo yao kwa jina la Yesu!.
Mimi ni Mtanzania na hii ndio nchi yangu, nitaendelea kuitii serikali yangu na kulitumikia Taifa langu kwa jina la Yesu!.
Mpaka sasa hivi, Serikali haijanidhuru kwa namna yoyote zaidi ya kunielekeza kwa kupewa maelekezo ya awali ambayo nayatekeleza kwa unyeyekevu mkubwa na akili, ustadi, hekima na maarifa pamoja na elimu niliyopewa na Mungu!.
Tutii, Kisha mengine yatafuata! Waliofurahia anguko langu pia wamenipa Funzo maana nilikuwa Naona sms zao na bado Nawaombea mema na afya njema kwao wote na wazidi kuwa imara katika kazi za mikono yao!.
Kazi ya Serikali ni kusimamia Sheria, Kanuni na ustawi wa watu wake, naamini, hapa narekebishwa ili niwe bora zaidi katika Taifa na dunaini kote kwa jina la Yesu!.
Asante Serikali yangu kwa kuwa Karibu na mimi, kinifuatilia, kunionya, kunifundisha na hatmaye kutaka niwe bora zaidi na nifanye kazi kwa ustadi pasipo kuathiri mambo mengine na jamii yangu!.
Nipo tayari kufundishwa, kuelekezwa kwa kusaidiwa na Serikali na Mungu wangu kwa jina la Yesu!.
AMINA
Nabii JAMES NYAKIA
030620251231
BRETHREN DEMONSTRATION POWER MINISTRY OF TANZANIA A.K.A SOJA MEGA ONE CHURCH
