CAIRO-Klabu ya Pyramids FC imeandika historia baada ya kutwaa taji la Klabu Bingwa barani Afrika (CAFCL), msimu wa 2024/25 kwa kuifunga Mamelodi Sundowns mabao 2-1 (3-2).
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la June 30 nchini Misri imeshuhudiwa Pyramids ikitwaa taji lake la kwanza la CAF tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa DR Congo, Fiston Mayele ameibuka mfungaji bora wa mashindano hayo kwa kufunga jumla ya mabao sita akimpita wa Al Ahly, Emmam Ashour mwenye mabao matano.