Rais Dkt.Mwinyi atoa ujumbe mahususi kuelekea Tamasha la Uwekezaji Zanzibar 2025

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha wawekezaji, wafanyabiashra na wananchi kwa ujumla kushiriki katika Tamasha la Uwekezaji Zanzibar (Zanzibar Investment Summit 2025) litakalofanyika kisiwani Pemba kuanzia Juni 15 hadi 17,2025.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito huo leo Juni 10,2025 kupitia ujumbe alioutoa kwa wananchi ambapo tamasha hilo linatarajiwa kuongeza fursa za ajira.

Pia,kukuza uchumi wa ndani na kuhamasisha uwekezaji wa kimkakati unaolenga kuinua maisha ya wananchi wa Pemba na Zanzibar kwa ujumla.

"Ndugu wawekezaji,wafanyabiashara,viongozi wa taasisi za umma na binafsi,waandishi wa habari na ndugu wananchi ni heshima kubwa kuwakaribisha kwenye tamasha la Uwekezaji Zanzibar mwaka 2025 yaani Zanzibar Investment Summit 2025 linalotarajiwa kufanyika tarehe 15 hadi 17 Juni,2025 katika maeneo huru ya uwekezaji Micheweni Pemba lenye kaulimbiu Ni wakati wa Pemba sasa."

Rais Dkt.Mwinyi amesema, madhumuni makuu ya tamasha hilo ni kuzitangaza fursa za uwekezaji na kibiashara ikiwemo kuyatangaza maeneo ya utalii yaliyopo Pemba.

"Madhumuni haya yanaenda sambamba na azma na mikakati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kukifungua Kisiwa cha Pemba kiuchumi na kibiashara."

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema, tamasha hilo litazikutanisha taasisi za uwekezaji kutoka ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wawekezaji wa ndani na nje ya nchi,wafanyabiashara,wadau wa maendeleo na sekta binafsi.

"Na watapata fursa za kujadiliana kwa pamoja mbinu na mikakati ya kukuza uchumi wa nchi yetu, kadhalika kwa kuzingatia umuhimu wa afya za wananchi kupitia tamasha hili wananchi wa Pemba watapata fursa ya kupatiwa matibabu na dawa bila malipo."

Amesema kuwa,hiyo ni sehemu ya mchango wa utoaji huduma za jamii kupitia uwekezaji unaofanyika nchini.

"Karibuni sana kujumika nasi katika tamasha la Uwekezaji mwaka 2025,karibu pia tuungane kuijenga Zanzibar mpya yenye uchumi imara, ajira kwa vijana na maisha bora kwa kila mmoja wetu, Zanzibar imefunguka ni wakati wa Pemba sasa."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news