Rais Dkt.Mwinyi awasili jijini Dodoma

DODOMA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama wa mkoa huo leo, tarehe 27 Juni 2025.
Rais Dkt. Mwinyi atashiriki katika mkutano wa kulifunga Bunge la 12, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, atalihutubia Bunge hilo, Bungeni, Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news