DAR-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuongeza safari za treni kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kwa treni za EMU maarufu mchongoko kati ya Juni 27 hadi 28 mwaka 2025.
.jpeg)
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Juni 27, 2025 treni itaondoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam saa 1:20 usiku na Juni 28, 2025 treni itaondoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam saa 12:50 asubuhi.
“Ongezeko la safari hizi ni kukidhi mahitaji ya usafiri kwa wananchi na wadau mbalimbali wanaosafiri kutoka Dodoma kurejea katika maeneo yao hususan jijini Dar es Salaam na miji mingine baada ya kuhitimishwa kwa shughuli za Bunge,” imesema taarifa.
