Rais Dkt.Mwinyi awatakia wananchi sikukuu njema ya Eid Al Adha, atoa rai kwao

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anawatakia waumini wote wa Dini ya Kiislamu kheri na baraka za Sikukuu ya Eid Al Adha.
Rais Dkt. Mwinyi amewataka wananchi kuitumia Sikukuu hii kama fursa ya kukuza mshikamano, kutoa sadaka na kutenda mema kwa jamii, sambamba na kuongeza ibada na uchamungu.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa wananchi kusherehekea kwa amani na utulivu, huku wakizingatia matumizi salama ya barabara hasa kwa madereva wa vyombo vya moto kwa kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani.

Amesisitiza pia umuhimu wa wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao katika kipindi hiki cha sikukuu, ili kuhakikisha usalama na maadili vinaendelea kupewa kipaumbele.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news