ARUSHA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeungana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kushiriki Maonesho ya Utalii ya Karibu-Kilifair 2025, yanayofanyika katika viwanja vya Magereza, jijini Arusha kuanzia tarehe 06 hadi 08 Juni.

Katika maonesho hayo, Benki Kuu imeweka msisitizo maalum kwenye Kanuni za Matumizi ya Fedha za Kigeni za Mwaka 2025, ambazo zinalenga kuimarisha uthabiti wa thamani ya Shilingi ya Tanzania ili kuchochea maendeleo endelevu ya uchumi na kuhakikisha ustawi wa taifa kwa ujumla.