DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na juhudi za kuimarisha utendaji katika serikali kwa kufanya mabadiliko, uteuzi na uhamisho wa Wakuu wa Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya katika maeneo mbalimbali nchini.
Katika mabadiliko hayo, Solomon Itunda amehamishwa kutoka Wilaya ya Songwe kwenda Mbeya. Japhari Mghamba amehamishwa kutoka Handeni kwenda Gairo, huku Amir Mkalipa akihamishiwa kutoka Arumeru kwenda Ilemela.Sambamba na hilo, Rais Samia amewateua Wakuu wa Wilaya wapya akiwemo Estomin Kyando kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Ayubu Sebabile (Muheza), Thecla Mkuchika (Butiama), Angelina Lubela (Serengeti), Maulid Dotto (Mvomero), Rukia Zuberi (Mwanga), Mwinyi Mwinyi (Arumeru), na Jubilete Lauwo (Magu).
Wengine walioteuliwa ni Mikaya Dalmia (Kigamboni), Thomas Myinga (Sikonge), Gloriana Kimath (Monduli), Upendo Wella (Tabora), Denis Masanja (Tunduru), Fadhil Nkurlu (Songwe), Benjamin Sitta (Iringa), Salum Nyamwese (Handeni), na Frank Mkinda (Kahama).
Aidha, Rais Samia ameteua makatibu tawala wa wilaya katika maeneo mbalimbali. Walioteuliwa ni Mwanamwaya Kombo (Mkinga), Kassim Kirondomara (Biharamulo), Thobias Abwaro (Babati), Asycritus Egaruk (Meatu), Nyakaji Mashauri (Kilolo), Mustapha Kimomwe (Rufiji), Milama Masiko (Serengeti), na Mpampalika Mpampalika (Mwanga).