Rais Dkt.Samia ateua viongozi mbalimbali

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika nyadhifa za kitaifa na kidiplomasia pamoja na kumpangia kituo cha kazi Balozi mmoja.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 16, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo unahusisha nafasi tano tofauti.

Dkt. Delilah Charles Kimambo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kuchukua nafasi ya Prof. Mohamed Yakub Janabi ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.

Viongozi wengine walioteuliwa ni Jaji Mstaafu Hamisa Hamis Kalombola kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha pili, na Paul Thomas Sangawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa SELF kwa kipindi cha pili pia.

Aidha, Jaji Rose Ally Ebrahim ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal), huku Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akipangiwa kituo cha kazi kama Balozi wa Tanzania nchini Italia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news