ARUSHA-Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeshinda mashauri ya madai na usuluhishi kwa niaba ya Serikali na taasisi zake katika kipindi cha mwezi Julai,2024 hadi Mei,2025 na kuokoa fedha ambazo Serikali ingelipa iwapo ingeshindwa mashauri hayo.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na Mawakili wa Serikali wakati wa Mafunzo kwa Mawakili hao kwa lengo la kuwajengea uwezo yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia Juni 2,2025 hadi Juni 4,2025.
Hayo yameelezwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt.Ally Possi wakati wa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali yaliyofunguliwa rasmi na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro Juni 3,2025 katika Ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) jijini Arusha.
Tags
Dkt.Ally Possi
Habari
Mawakili wa Serikali
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
Wakili Mkuu wa Serikali




