Wataalamu wa TEHAMA wa Sekta ya Maji watakiwa kuhakikisha mifumo inasomana

DODOMA-Wataalamu wa TEHAMA katika Sekta ya Maji kuongeza nguvu katika kuhakikisha mifumo ya kidigiti inasomana kuendana na teknolojia inavyokua.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amesema hayo Mtumba, jijini Dodoma na kuongeza kuwa hatua hiyo itarahisisha kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma ya maji kwa haraka.
Akiongea na wataalamu hao amewataka kutafuta namna bora itakayowezesha upatikanaji wa taarifa muhimu kuhusu masuala ya huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kupitia mifumo.
"Hakuna sababu ya kuanza kuzitafuta taarifa za hali ya huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwenye makaratasi au kwa watu, haya yanaweza kufanyika kupitia mifumo iliyo jitosheleza,” Mhandisi Mwajuma amesema.
Pamoja na hilo, awamewapongeza wataalamu wote kwa jitihada wanazo zifanya katika kuhakikisha lengo na mkakati wa Wizara ya Maji yanafanikiwa kupitia TEHAMA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news