Super Brand yaipaisha Simba SC tena

DAR-Taasisi ya Super Brand imeitangaza klabu Simba SC ya jijini Dar es Salaam kuwa chapa (brand) bora namba moja ya michezo nchini katika kipindi cha mwaka 2024 hadi 2026.
Simba SC imekuwa kinara nchini kwa upande wa taasisi za michezo, lakini imeshika nafasi ya pili kwa ujumla miongoni mwa taasisi 10 bora zilizopewa hadhi ya Super Brand.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi hiyo baada ya kuulizwa wananchi 1000 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha wote wamekiri kuwa Simba ni chapa bora kwa sasa nchini.

Super Brand wamekuwa wakifanya tafiti hizo kila mwaka kwa taasisi mbalimbali nchini ikiwa na lengo la kuhamasisha ufanyaji kazi kwa ufanisi ili kuleta matokeo chanya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Doreen Bangapi amesema, lengo la kutambua taasisi hizo ni kuongeza chachu katika kutimiza majukumu kwa ufanisi mkubwa na thamani yao kutambuliwa nchini.

“Leo tupo hapa kwa ajili ya kutaja Taasisi 10 bora ambazo zimepewa hadhi yakuwa Super Brand kutokana na utendaji wake katika kipindi cha mwaka 2024-25,” amesema Bi. Doreen.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo imefanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam ambapo kwa upande wa klabu imepokelewa na Meneja Uendeshaji, Bi. Belinda Paul.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news