SIMIYU-Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo, amewataka wakulima Mkoa wa Simiyu kubadilika na kuanza kutumia mbinu bora za kilimo zikiwemo matumizi sahihi ya mbolea ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo akizungumza na wakulima wa kijiji cha Bubalabujiga Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu na kuwataka kubadili mitazamo yao kuhusu matumizi ya mbolea ili wawezekuzalisha kwa tija na kuongeza vipato vyao tarehe 12 Juni, 2025.Dkt. Diallo ametoa wito huo nyakati tofauti tarehe 12 na 13 Juni 2025, alipokuwa akizungumza na wakulima wa vyama vya msingi vya Ushirika na wakulima wa mazao ya Pamba na Mahindi wa wilaya za Itilima, Meatu na Maswa Mkoani Simiyu wakati wa ziara ya bodi na menejimenti ya TFRA iliyolenga kuhamasisha matumizi ya mbolea mkoani humo.
Akisisitiza umuhimu wa matumizi ya mbolea, Dkt. Diallo ameeleza kuwa, matumizi sahihi ya mbolea yatawafanya wakulima kuongeza uzalishaji na kulima eneo dogo la ardhi na hivyo kupunguza migogoro ya ardhi inayotokana na uhitaji wa mashamba makubwa wakati huohuo uzalishaji wake kutokuwa wa kuridhisha.
Wananchi wa kijiji cha Mbugamita kata ya Senani wilayani Maswa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo (hayupo pichani) alipokuwa akiwahamasisha kutumia mbolea na kubadilisha mitazamo kuhusu mbolea ili kuongeza tija kwenye kilimo chao tarehe 13 Juni, 2025.
Wananchi wa kijiji cha Mbugamita kata ya Senani wilayani Maswa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo (hayupo pichani) alipokuwa akiwahamasisha kutumia mbolea na kubadilisha mitazamo kuhusu mbolea ili kuongeza tija kwenye kilimo chao tarehe 13 Juni, 2025.“Mkulima anaweza kulima ekari tatu tu na kufanikisha mahitaji yake ya chakula na kipato badala ya kulima maeneo makubwa bila tija,” anasema Dkt. Diallo.
Aidha, Dkt. Diallo ameeleza kuongezeka kwa kipato kwenye kaya zao kutapunguza wimbi la vijana kukimbilia mijini na kufanya kazi zisizokuwa na tija na kuwaingiza katika makundi yasiyofaa.
Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), CPA. John Cheyo akizungumza na wakulima wa kijiji cha Mbugamita Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wakati wa ziara ya bodi na menejimenti ya Mamlaka iliyofanyika tarehe 12 na 13 Juni, 2025 ili kuhamasisha wakulima wa mkoa huo kutumia mbolea kwenye kilimo na kuongeza tija.Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti TFRA, Bi Elizabeth Bolle akiwahamasisha wakulima wa kijiji cha Mbugamita Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu kulima kisasa kwa kutumia mbolea ili wazalishe kwa tija na kuongeza kipato chao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa TFRA, Bi. Elizabeth Bolle, ameeleza kuwa, lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha matumizi ya mbolea ili kuongeza tija kwa wakulima pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili ili zitatuliwe kwa wakati na kuwafanya wakulima kuinua uchumi wao.
Naye, Mkaguzi wa Pamba kutoka Bodi ya Pamba Tanzania, Bw. Daniel Bariyanka, amewahimiza wakulima kuwatumia wataalam waliopo katika maeneo yao, ikiwemo washauri wa kilimo wa mpango wa BBT, ili wapewe elimu ya kanuni bora za kilimo cha pamba na mazao mengine.
Wananchi wa Kijiji na Kata ya Bubalabujiga wilayani Itilima wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo (hayupo pichani) alipokuwa akiwahamasisha kutumia mbolea na kubadilisha mitazamo kuhusu mbolea ili kuongeza tija kwenye kilimo chao tarehe 12 Juni, 2025.
“Bei ya pamba kwa sasa ni nzuri ukilinganisha na nchi jirani, lakini ili kufikia masoko ya uhakika na kupata faida kubwa, ni lazima tulime kwa tija na kutumia mbolea,” amesema Bariyanka.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao na bodi katika kijiji cha Bubalabujiga wilayani Itilima mkulima, Leticia Matanga, ameishukuru Bodi ya Mamlaka kwa kupeleka elimu hiyo muhimu na kuiomba iendelee kutoa elimu na kuwahamasisha wakulima kutumia mbolea ili kubadilisha maisha yao.
"Kwa muda mrefu tumekuwa tukilima pamba bila kutumia mbolea na kuvuna kilo 250 kwa ekari moja, lakini leo tumejifunza kuwa, tukitumia mbolea tunaweza kuvuna zaidi ya kilo 1,000.
Vilevile, tumeelezwa kuwa, mahindi tunayovuna gunia 5 hadi 7 kwa ekari yanaweza kufikia gunia 30 hadi 35 tukitumia mbolea," alisema Matanga.
Wakulima wa Wilaya ya Itilima waliiomba Serikali kupitia TFRA na wadau wengine wa kilimo kuendelea kutoa elimu endelevu kuhusu matumizi bora ya mbolea pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa mbolea katika maeneo yao kwa wakati na kwa bei nafuu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mbugamita kata ya Senani wilayani Maswa wakati wa ziara ya bodi na Menejimenti ya TFRA ya kuhamasisha wakulima kutumia mbolea na kubadilisha uchumi wao kwa kuongeza tija kwenye kilimo chao tarehe 13 Juni, 2025.“Tunaomba elimu hii iendelee kutolewa mara kwa mara, na mawakala wasogezwe karibu na maeneo yetu ili tuweze kupata mbolea kwa urahisi.






